Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali kupitia wizara ya elimu imetenga shilingi bilioni 16 zitakazotumika kujenga vyuo vya kiufundi katika maeneo bunge 290 kote nchini katika kipindi cha mwaka wa fedha ujao.

Waziri wa elimu Dkt Fred Matiang'i aliyathibitisha haya alipokuwa akiyatangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne KCSE katika jumba mtihani mjini Nairobi siku ya Alhamisi.

Matiang'i alisema kuwa vyuo hivyo vitatoa nafasi kwa zaidi ya wanafunzi 290,000 kote nchini waliokosa alama za kujiunga na vyuo vikuu kuendelea na masomo yao.

Aidha waziri huyo, alisema kuwa ni thuluthi moja tu ya wanafunzi waliofanya mtihani wa mwaka jana ndio watapata nafasi ya kujiunga moja kwa moja na vyuo vikuu vya humu nchini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu elimu, Sabina Chege, aliwahimiza wanafunzi watakaokosa fursa ya kujiunga na vyuo vikuu kujisajili na vyuo vya kiufundi.