Mahakama ya Kisii imeagiza chama cha Orange Democratic Party (ODM) kutomtangaza Joshua Maaga kama mwenyekiti katika eneo bunge la Bomachoge Borabu kaunti ya Kisii hadi kesi iliyofikishwa katika mahakama hiyo isikizwe na kuamuliwa.
Kesi hiyo inapinga kuchaguliwa kwa Maaga kama mwenyekiti kwa madai kuwa stakabadhi za vyama nchini zinaonyesha yeye ni mwanachama wa chama cha UDF na wala si ODM.
Mnaomo siku ya Alhamisi jaji wa mahakama hiyo ya Kisii Ruth Maroba aliagiza chama cha ODM kusitisha hatua ya kumtangaza Maaga kama mshindi hadi swala hilo litatuliwe.
Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani na Joseph Nyandieka, Samuel Okemwa, Fidelis Ombori na Evans Okengi kupitia wakili wao Philemon Ochiengi.
“Joshia Maaga hatakubaliwa kuwa mwenyekiti hadi kesi iliyo katika mahakama hii isikizwe na kuamuliwa,” jaji Maroba alisema.
Kesi hiyo itasikizwa tena Januari 7, 2016.