Dereva wa matatu moja alifikishwa mahakamani Nakuru Jumatatu na kushtakiwa kwa kusababisha ajali iliyofanya watu wane kupoteza maisha yao.
Mahakama ilielezwa kuwa mshukiwa alitekeleza ajali hiyo na kasha kutoweka.
Hata hivyo, mshukiwa alikanusha madai hayo akisema kuwa ajali hiyo ilimfanya kupoteza fahamu na hivyo hakujua kilichotendeka.
Mbele ya jaji Liz Gicheha, mshukiwa alisema alipata fahamu akiwa kwenye hospitali kuu ya kaunti.
Kesi hiyo itaendelea Machi 23, 2016.