Kiongozi wa wachache katika bunge la kaunti ya Baringo ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya Mukutano alifikishwa mahakamani kwa madai ya kuchochea ghasia kati ya Jamii za Ilchamus na Tugen huku watu watatu wakifariki.
Mwakilishi huyo wa wadi Renson Parkia alifikishwa mahakamani Jumatatu akidaiwa kuwa mnamo tarehe moja mwezi Februari katika kijiji cha Olesampurur kwenye kaunti ndogo ya Baringo Kusini alitamka maneno ya uchochezi.
Hata hivyo, Parkia aliyefikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Nakuru Liz Gicheha alikana shtaka hilo na kuwachiliwa kwa bondi ya shilingi elfu mia tano na mdhamini wa kiasi sawa.