Mwenyekiti wa Grassroot Women Empowerment Grace Kibuku ametangaza rasmi kuwania kiti cha mwakilishi wa wanawake kaunti ya Nakuru katika uchaguzi mkuu ujao.
Katika mahojiano ya kipekee, Kibuku, ambaye aliwai wania wadhifa huo 2013 bila mafanikio amesema kuwa wakati huu amejipanga vilivyo.
Isitoshe ameongeza kuwa wakazi wa Nakuru wamejionea wenyewe na watafanya maamuzi bora mwaka ujao.
"Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo na mi najua wakazi wa Nakuru miaka mitano hii wamejifunza mengi na wakati ni sasa wa kufanya maamuzi bora," alisema Kibuku.
Wakati huo huo, balozi huyo wa tuzo la Rais la amani amewataka wakenya kuwa watulivu na kujiandikisha kama wapiga kura. Kwa mujibu wake, viongozi fisadi wataondolewa tu afisini kupitia kura.