Mwanamume mmoja alifikishwa katika Mahakama ya Winam jijini Kisumu siku ya Jumatatu kujibu shtaka la ulanguzi wa dawa za kulevya.
Upande wa mashtaka uliambia mahakama kuwa mshtakiwa, Victor Otieno, anadaiwa kunaswa na lita 40 za pombe haramu aina ya chang'aa na misokoto 18 ya bangi jijini Kisumu, mnamo tarehe 11 mwezi Februari mwaka 2012.
Pombe hiyo pamoja na bangi, viliwasilishwa mbele ya mahakama kama ushahidi.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikanusha mashtaka hayo.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe tano mwezi Mei, ambapo uamuzi unatarajiwa kutolewa.