Idadi ya wagomjwa wanaofariki kutokana na maradhi ya kifua kikuu kaunti ya Mombasa imepungua kutoka asilimia 10 hadi asilimia 3.1 kwa mwaka.
Akizungumza kwenye mkutano na wadau wa afya mkuu wa huduma ya kifua kikuu na ukoma kaunti ya Mombasa Samson Kioko amesema kuwa kufuatia uhamasisho kuhusu maradhi hayo na pia wagonjwa kuzingatia taratibu za utumiaji wa dawa kumesaidia kupunguwa kwa ugonjwa huo.
Siku ya Alhamisi, Kioko alisema wengi walioshikwa na TB sugu wamepokea matibabu na kupona, huku watu 27 wakiwa bado wanaendelea na tiba hiyo ambayo huchukua muda wa miezi 20 kutibiwa.
Adha, alidokeza kuwa eneo bunge la Kisauni linaongoza kwa maradhi hayo ya kifua kikuu ikifuatwa na eneo bunge la Mvita, Changamwe na Likoni.
Ameongeza kuwa sababu ya maambukizi hayo ni kutokana na maisha duni, upangaji mbaya wa nyumba na msongamano wa watu.