Watu wanne waliepuka kifo Alhamisi baada ya lori waliyokuwa wakisafiria kupingilia mara kadhaa katika eneo la White House viungani mwa mji wa Nakuru.
Lori hilo ni la kampuni moja ya kibinafsi ambayo imepewa kandarasi na serikali ya jimbo la Nakuru kutoa huduma za kuokota takataka.
Punde baada ya kubingiria, lori hilo lilianza kuwaka moto na kuwalazimu wakaazi kuuzima haraka kwa maji ili kuwaokoa wanne hao.
Manusura hao hata hivyo walipelekwa kupokea matibabu katika hospitali ya Nakuru Level Five na kuruhusiwa kuondoka.
Mkaazi Lydia Wairimu alisema kuwa ajali hiyo ilichangiwa na hali duni ya barabara ya Maragoli.