Wakazi wa Kebirigo hasa wafanyibiashara wakuuza bidhaa za rejareja wanaendelea kukadiria hasara ya mamillioni ya pesa baada ya moto kuteketeza mali yao usiku wakuamkia siku ya Jumatatu.
Akithibitisha kisa hicho OCPD wa Nyamira Ricoh Ngare alisema huenda moto huo ulisababishwa na hitilafu za nguvu za umeme, ila uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo chake.
"Inakisiwa kuwa huenda moto huu ulisababishwa na hitilafu za nguvu za umeme ila tumeanzisha uchunguzi kubaini ukweli wa mambo," alisema Ngare.
Juhudi za wazima moto kutoka kaunti jirani ya Kisii kukabili moto huo ulioanza mwendo wa saa tatu usiku siku ya Jumapili ziliambulia patupu baada ya wazima moto hao kufika kwenye tukio nusu saa baada ya tukio hilo kujiri.