Mrengo wa Cord umesitisha maandamano dhidi ya Tume ya IEBC kwa muda.
Kulingana na mrengo huo, hatua hiyo ni njia mojawapo ya kutoa nafasi kwa serikali ya Jubilee kuandaa mazungumzo ya kushughulikia matakwa yao.
Mrengo huo umeipa serikali ya Jubilee hadi tarehe tano mwezi Juni, kuwabandua baadhi ya maafisa wa IEBC la sivyo wataendelea na maandamano hayo kote nchini.
Maandamano ya Cord mjini Mombasa siku ya Jumatatu yalipelekea baadhi ya viongozi wa kaunti kujipata mikononi mwa serikali, huku wafuasi wanne wakiripotiwa kufariki katika Kaunti za Kisumu na Siaya.