Spika wa bunge la kaunti ya Kisii Okerosi Ondieki amewahimiza wakaazi wa kaunti hiyo ya Kisii kujitokeza kila wakati kutoa maoni yao kuhusu bajeti ya kila mwaka na miradi mingine ambayo hufanywa na serikali ya kaunti hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa bajeti hutolewa na miradi mingine hufanywa bila wakaazi kujitokeza ili kutoa maoni yao kisha baadaye wananza kulalama wakisema serikali ya kaunti inawakandamiza na kufanya mengi bila kuwahusisha jambo ambalo Ondieki alisema halistahili kushuhudiwa katika kaunti ya Kisii

Akizungumza siku ya Jumapili mjini Kisii, Ondieki alisema ni muhimu kwa wakaazi kujumuishwa kwa kila jambo linalofanywa na serikali ya kaunti ili kuonyesha uwazi kwa kila jambo.

“Kaunti yetu haitaki kupuuza maoni ya wakaazi maana ndio walichagua viongozi wa kufanya maendeleo, naomba wakaazi wa Kisii wanapoitwa kutoa maoni ya bajeti na miradi mingine ya serikali wawe wanajitokeza ili kutoa mchango wao,” alisema Ondieki.

Ondieki alisema katiba inaruhusu wakaazi kuhusishwa kwa miradi ya maendeleo na katika utengenezaji wa bajeti