Akina mama katika Kaunti ya Nyamira wameshauriwa kupimwa ugonjwa wa saratani ya mfuko wa kizazi ili kupata matibabu mapema iwapo watapatikana na ugonjwa huo.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika Hospitali ya Manga, Shirika la International Medical Scoop lilipokua linakabidhi kaunti ya Nyamira mashine za kupima ugonjwa huo, mkuu wa idara ya afya katika kaunti ya Nyamira Gladys Momanyi aliwahimiza wanawake kuenda hospitalini kupimwa ugonjwa huo ili kujua hali zao baada ya kila miezi miwili.
“Tuligundua kuwa baadhi ya wanawake huogopa kujitokeza na kufika hospitalini ili kupimwa ugonjwa wa saratani ya mfuko wa uzazi. Naomba akina mama kutoogopa na mjitokeze kujua hali zenu,” alisema Momanyi.
Aliongeza, “Ata mtoto wa umri wa miaka 12 anaweza ugua ugonjwa huo wa saratani ya mfuko wa uzazi na naomba kila mwanamke, ata watoto ambao wamefikisha zaidi ya miaka 12, kuenda hospitalini ili kupimwa ugonjwa huo.”
Shirika hilo la International Medical Scoop kilikabidhi serikali ya kaunti ya Nyamira Mashine tatu za kupima ugonjwa huo wa saratani ya mfuko wa kizazi.
Momanyi alisema mashine hizo zitawasilishwa katika Hosptali za Kijauri, Ekerenyo na Manga.