Huku joto la kisiasa likionekana kupamba moto, Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, imehimizwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu bila kuegemea upande wowote.
Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, afisa mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Africa Francis Auma amesema kuwa ni jukumu la tume hiyo kujitenga na siasa za vyama ili kuhakikisha kwamba uchaguzi mkuu wa Agosti utakua wa huru na haki.
Auma aidha alisema kwamba ipo haja ya tume hiyo kuzidisha hamasa zaidi miongoni mwa wananchi.
Alisema kuwa wananchi wanapaswa kuelimishwa kuhusu jinsi ya kupiga kura, ili kuzuia visa vya kura kuharibika.
Hata hivyo, amewataka wananchi kujitenga na siasa zitakazoleta mgawanyiko miongoni mwao.
Auma amewahimiza Wakenya kudumisha amani ili kuepuka visa vya vurugu ifikapo wakati wa uchaguzi.
Alisema itakua jambo la kusikitisha iwapo kutashuhudiwa machafuko ya baada ya uchaguzi kama yale ya mwaka wa 2007/2008.