Mke wa gavana wa kaunti ya Nyamira Naomi Nyagarama amewahimiza kina mama wajawazito kuhakikisha kuwa wanajifungulia hospitalini. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiwahutubia wakazi wa eneo la Ekerenyo siku ya Almahisi wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya kifua kikuu ulimwenguni, Nyagarama alisema kuwa yastahili kina mama wajawazito wawe na mazoea ya kujifungulia hospitalini kwa minajili ya usalama wao na wanao. 

"Kuna uwezekano mkubwa kwamba maisha ya mama mjamzito ambaye labda ana matatizo ya kujifungua yanaweza kuokolewa iwapo atajifungulia hospitalini kuliko nyumbani, kwa maaana uangalizi kwenye hospitali ni wa hali ya juu na ndio sababu nawahimiza kina mama kuwa na mazoea ya kujifungulia hospitalini," alisema Nyagarama. 

Aidha aliwahimiza kina mama wajawazito kukumbatia huduma za gari la kliniki tamba ili iwe rahisi kwao kupata huduma kwa haraka. 

"Kuna hili gari la kliniki tamba ambayo Bi. Magret Kenyatta alitupokeza na ni nzuri sana kwa utoaji huduma kwa haraka hasa kwa kina mama wajawazito kwa maana gari hilo ni kama hospitali inayotembea, na ndio maana nawahimiza wakazi wa kaunti hii kukumbatia huduma zake," aliongezea Mkewe gavana.