Mwanamke wa umri wa makamo ameuawa na wakaazi wa Soko Mjinga, Kisauni kwa tuhuma za kuwa mchawi.
Mshikemshike ulianza baada ya mwanamke huyo kudaiwa kupatikana juu ya paa ya nyumba moja akiwa uchi.
Inaripotiwa kuwa wakaazi walimchoma mwanamke huyo kwa magurudumu ya gari yaliyotiwa mafuta ya petroli, huku wenzake wawili wakitokomea gizani.
"Mwanamke huyo alikuwa uchi kabisa wakati wa tukio hilo, kisa kilichomfanya kushambuliwa na wakaazi waliomshuku kuwa mchawi,” alisema mkaazi mmoja.
Wakaazi wa eneo hilo walidai kuwa mwanamke huyo amekuwa kizingiti kwa kuwa amekuwa akiwahangaisha sana.
Wakaazi hao walisema kuwa waliamua kumshambulia mwanamke huyo baada ya kushindwa kueleza wazi ni nini haswa alikuwa akifanya juu ya paa hilo huku akiwa uchi wa mnyama.