Mshukiwa aliyehusika na ulipuzi wa hoteli ya Bella Vista ,Thabith Jamaldin Yahya amehukumiwa kifo na mahakama kuu ya Mombasa.
Thabith Jamaldin Yahya anahusishwa na ulipuzi wa hoteli hiyo na kusababisha kifo cha mlinzi wa hoteli hiyo Mary Cheptrim mnamo Mei 15 , 2012.
Siku ya Alhamisi, jaji Martin Muya ,alisema kuwa kulingana na ushahidi ni wazi mshukiwa alihusika katika ulipuzi huo na kumuhukumu kifo.
Thabith amesalia rumande tangu kutiwa mbaroni kwake mwaka 2012.
Thabith Jamaldin Yahya yuko na siku 14 za kukata rufaa.