Wakaazi wa eneo bunge la Kilifi Kusini wametishia kumuondoa mamlakani mbunge wao Mustapha Idd kwa maadai kuwa hajatekeleza maendeleo yoyote katika eneo hilo na kusema kuwa hawajafurahishwa na hatua yake ya kugura chama chake cha ODM.
Mohammed Yusuf ambaye ni mkaazi wa eneo hilo amesema kuwa huenda wakawasilisha ombi kwa taasisi za kisheria ya kutaka uchaguzi mdogo ufanywe katika eneo bunge hilo.
Aidha, Leah Aketch ambaye pia ni mkaazi wa eneo hilo amesema kuwa hakuna maendeleo ambayo yamefanyika katika eneo hilo huku akilalamikia hali mbaya ya barabara na ukosefu wa hospitali katika eneo hilo.
Wakaazi hao walisema haya siku ya Alhamisi walipoandaa maandamano ya amani katika eneo hilo na kusema kuwa wamempa mbunge huyo miezi miwili kuwashirikisha katika mazungumzo.