Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Idara ya polisi kaunti ya Mombasa imelaumiwa pakubwa kutokana na visa vya mara kwa mara vya maduka ya Mpesa kuporwa na wahalifu eneo la Kisauni Mjini Mombasa.

Wahudumu hao wamesema kuwa vijana wa umri mdogo wanaotumia dawa za kulevya huzurura nyakati za usiku na kuwapora wahudumu hao wakati wakijitayarisha kufunga biashara zao na kutoweka na pesa ama mapato ya siku.

Aidha kulingana na Philip Karisa ambaye ni mmoja wa wahudumu wa Mpesa vijana hao wenye umri wa kati ya miaka kumi na mitano hadi ishirini hutembea usiku huku wengine wakirauka saa nane usiku na kukata sehemu za madirisha ya nyumba na kutoa vitu vidogovidogo kama vile simu huku wenyewe wakiwa wamelala.

Kwenye kisa cha hivi punde mhudumu mmoja wa Mpesa alishtukizia vijana wenye panga kwake nyumbani ambao walimnyakua kibeti chake kilichokuwa na mali ya biashara ya siku.

Wahudumu hao sasa wanasema kwamba huenda vijana hao wakawa wanashirikiana na baadhi ya wakaazi eneo hilo wanaowafahamisha duka la kutekeleza uhalifu huo.