Wananchi wametajwa kuchangia kukithiri kwa kashfa za ufisadi katika idara mbalimbali za serikali na mashirika binafsi kutokana na wananchi wenyewe kuwatetea wahusika wakuu wa kashfa za ufisadi.
Katibu mkuu wa baraza la Maimamu na Wahubiri wa humu nchini CIPK, Sheikh Mohammed Khalifa amesema kuwa lazima wananchi kujitenga na viongozi wafisadi na wale wanyanyasaji wananchi na kuwashinikiza kurudisha mali ya umma basi kwa kiasi kikubwa ufisadi utasitishwa nchini.
Akiongea na mwanahabari huyu mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Sheikh Khalifa amesema kuwa kamwe ufisadi nchini hautakabiliwa kutokana na wananchi wenyewe kuchangia ufisadi na hata kuwatetea viongozi wafisadi mahakamani huku akisema kuwa iwapo wananchi watakubali kubadili hali ya uongozi nchini basi ufisadi utakomeshwa.
"Ufisida nchini kamwe hatutasitishwa kutokana na kuwa wananchi wenyewe ndio wanaochangia kukithiri kwa ufisadi kufuatia kuwaunga mkono na kuwatetea viongozi wanaodaiwa kuwa wafisadi kuambana na kuwa ati mfuasi wao ananyanyaswa huo ni unyanyasaji wa kwanza na ufisadi kamwe hautaisha," alieleza Sheikh Khalifa.
Hii inajiri baada ya tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC kutaja kaunti zinazofuja fedha za umma.