Share news tips with us here at Hivisasa

Washukiwa wawili wa ujambazi wamefikishwa katika mahakama moja jijini Kisumu siku ya Alhamisi wakikabiliwa na shtaka la wizi wa kujihami.

Upande wa mashtaka umefahamisha mahakama kuwa Moses Omondi Otiang na Saumu Khadijah Abira walivamia duka la mlalamishi Leornad Bahati Simiyu lililoko katika jengo la duka la ujumla Tuskys jijini Kisumu.

Imearifiwa kuwa katika uvamizi huo wa tarehe November 17, 2015, wawili hao wakiwa wamejihami kwa bunduki aina ya pistol walivamia duka la mlalamishi mwendo wa saa nane mchana na kutoweka na simu ya shilingi alfu 5 na kiasi cha shilingi 148,000.

Wakiwa mbele ya hakimu, Angeline Adawo mshtakiwa Moses Omondi alikiri mashtaka dhidi yake ila Saumu alikanusha mashtaka dhidi yake.

Kesi hiyo imeratibiwa kusiklizwa tarehe Marchi 11, 2016.