Afisaa wa polisi tawala alijeruhiwa asubuhi Alhamisi wakiwa katika operesheni ya kuwasaka majambazi waliotekeleza mashambulizi katika mtaa wa Flamingo viungani mwa mji wa Nakuru.
Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa utawala mjini Nakuru Barnabas Kimutai, afisaa huyo kwa jina la Erustus Opicho alianguka kutoka kwenye gari la polisi lililokuwa likiwafukuza baadhi ya washukiwa wa genge ambalo lilikuwa linajiandaa kulipiza kisasi, kufuatia kushambuliwa kwa vijana wawili hapo jana jioni katika mtaa wa Flamingo kwa jina la Kenneth Mukangale na Geoffrey Mungai.
Afisaa huyo alikimbizwa katika hospitali Langalanga viungani mwa mji wa Nakuru.