Kitengo cha trafiki katika kaunti ya Nakuru kimesema kuwa watafanya msako wa bodaboda zote zinazovunja sheria na kusababisha ajali kuongezeka.
Polisi walisema kuwa ukosefu wa kuvalia kofia za usalama na kutozingatia sheria zilizowekwa barabarani kumechangia pakubwa kuongezeka kwa ajali zinazosababishwa na pikipiki hizo.
Kamanda wa polisi katika kaunti ya Nakuru Hassan Barua amesema bodaboda zimekuwa zikivunja kanuni za barabarani.
“Tutafanya msako huo wakati wowote na wale watakaopatikana watashtakiwa na kupoteza leseni zao za kuhudumu," Baru alisema.
Kamanda huyo alikuwa akizungumza baada ya kufanya kampeini ya usalama wa barabara katika eneo la Kinungi kwenye barabara kuu ya Nairobi kwenda Nakuru.
Naye msimamizi wa mamlaka ya kusimamia babarabara kuu nchini (KeNHA) Ezekiel Fukwo alisema: “Tumeweka mikakati maalum ili kuhakikisha kuwa ajali zimepungua wakati huu wa sherehe nyingi."