Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi kutoka kituo cha kibiashara cha Heshima na maeneo ya karibu kaunti ya Nakuru, wamesifia huduma bora kutoka kwa wahudumu wa afya na madaktari wa kliniki tamba chini ya kampeni ya Beyond Zero.

Jumanne wakaazi wasiopungua 200 wa Heshima, Maili Sita, Kagoto, Kwa-Buda na Stoo Makaa eneo bunge la Bahati, walipata tiba za bure kutoka kwa wahudumu wa kliniki hiyo.

Mkaazi John Kariuki, alisafiri kilomita nne kutoka Section 58 kufika Heshima, ili kupata huduma hizo baada ya kuumwa na tumbo kwa zaidi ya wiki moja.

“Nimeridhika na huduma ambayo nimepata, japo laini imekuwa ndefu kutokana na wingi wa watu” alisema Bw Kariuki.

Wengi wa waliofika kupokea huduma hiyo walikuwa akina mama, kulingana na mhudumu aliyeomba kutotajwa jina.

Hata hivyo katika mahojiano na mwandishi huyu, wengi wa waliokuwa wakitafuta huduma hizo walisema kwamba umaskini unachangia watu kushindwa kupata matibabu bora.

Kliniki hiyo ya Beyond Zero inafuatia kampeni aliyozindua mama wa taifa, Bi Margaret Kenyatta.