Kijana mwenye umri wa makamo ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili kwa kosa la kupatikana na mali ya wizi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Upande wa mashtaka umeiambia mahakama kuwa, mnamo Machi 15, 2016, mshukiwa Kahindi Said Mwero, anadaiwa kupatikana na gurudumu la gari lenye thamani ya shilingi 50,000.

Siku ya Alhamisi, Kahindi alikanusha madai hayo mbele ya hakimu mkuu katika mahakama ya Mombasa, Susan Shitub.

Kesi hiyo itasikilizwa Mei 17, 2016.