Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali ya Kaunti ya Kisii imeombwa kuongeza mataa ya uslama katika soko la Nyakongo katika eneo bunge la Kitutu Chache ili kuimarisha usalama katika soko hilo haswa nyakati za usiku.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano katika soko hilo, wafanyibiashara wa soko hilo, wakiongozwa na mwenyekiti wao Cornellius Nyangenya waliomba serikali ya kaunti kuongeza mataa ili kuimarisha usalama kwa soko hilo kando na taa moja ambalo limewekwa kwa sasa.

Kulingana nao, idadi kubwa ya wafanyibiashara huacha bidhaa zao kwa soko hilo nyakati za usiku huku wakihofya kuwa huenda wezi wavunje milango na kutekeleza wizi nyakati za usiku, jambo ambalo limewafanya kuomba usiaidizi huo. 

“Ikiwa serikali inahitaji bidhaa zetu ziwe katika hali ya usalama, sharti iongeze mataa katika soko hili ili yawe mataa tatu au nne kwa usalama,” alisema Nyangenya.

Hapo awali Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae alitoa ahadi kuwa atajenga soko zote na kuziweka mataa ya usalama ili kutumika wakati wa usiku kwa usalama, jambo ambalo sasa linaongojewa kutekelezwa.