Mwenyekiti wa wabunge wa pwani Gunga Mwingi ameahidi kuwaunganisha viongozi wa pwani na kufanya kazi kwa pamoja ili kufanikisha maswala muhimu yanayomuhusu mkaazi wa pwani.
Gunga ambaye pia ni mbunge wa Kaloleni, amesema kuwa uteuzi ulifanywa siku ya Jumatano ilikuwa sawa kwa viongozi wote ili kuhakikisha viongozi binafsi wanabanduliwa kutoka nyadha hizo na kuwasaidia wapwani kupata mahitaji muhimu waliyokuwa wanahitaji.
Akiwahutubia wakaazi wa pwani katika harambee ya kuchangisha pesa siku ya Alhamisi, Gunga amesema kuwa jukumu la muungano huo ni kuhakikisha kuwa viongozi wa pwani na wakaazi wanaungana katika juhudi za kukabiliana na dhulma za kihistoria zilizochangia wakaazi wa pwani kusalia nyuma kimaendeleo.
Amesema kuwa unyanyasaji wa jinsia na unyakuzi wa ardhi katika eneo la pwani ndio swala ambalo muungano huo umeupa kipau mbele kuhakikisha kuwa wakaazi wa pwani wanapata haki sawa na kupata hati miliki za ardhi.
"Muungano huu umeonyesha wazi kuwa maswala tata ya dhulma za kihistoria na unyakuzi wa ardhi yatapiganiwa na kuwapa wapwani uhuru wa kumiliki ardhi zao sawa na hati miliki",alisema Gunga.
Sasa Muungano huo unasubiri kuona kuwa itakabiliana na ahadi walizoahidi baada ya kuchaguliwa siku ya Jumatano huku waliyokuwa wakishikilia nyadhfa hizo wakionekana kujitenga na muungano huo.
Mwenyekiti wa muungano wa wabunge wa pwani Gunga Mwing{wapili kushoto},Mbunge wa Rabai Willium Kamoti{kulia} pamoja na viongozi wengine wa pwani.