Vijana wengi wameombwa kujituma na kufanya kazi hata kama ni za vibarua ili kujipa riziki ya kila siku na wawe wakujitengemea.

Share news tips with us here at Hivisasa

Joseph Mwaura ni mwanaharakati wa maswala ya kisiasa kaunti ya Mombasa, amesema kuwa vijana katika mkoa wa Pwani wamejawa na fikra potovu za kuwa ni lazima waajiriwe ndio watafute mkate wao wa kila siku.

Mwaura ameongeza kuwa hali hii inafaa kubadilika na waanze kujituma ili waweze kubadilisha taasubi hiyo.

Aidha ameongeza kusema kuwa idadi kubwa ya vijana huingia kwenye maswala ya kujihusisha na kubugia mihadarati na visa vya uhalifu.

Hatahivyo, amesema kuwa kupitia uwezo wake na wizara ya vijana ya serekali ya kaunti, atashirikiana nayo na kuhakikisha kuwa hali hiyo imerekebishwa kupitia ushauri nasaha.