Vijana wameonywa dhidi ya kutumiwa na wanasiasa kuleta vurugu kila wakati katika mji wa Keroka kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Onyo hilo limetolewa baada ya kubainika kuwa kuna baadhi ya wanasiasa ambao wanatumia vijana kuleta mzozo katika mpaka ulioko mjini Keroka kati ya kaunti ya Kisii na ile ya Nyamira
Akizungumza siku ya Alhamisi mjini Keroka, Mkuu wa polisi katika kituo cha Keroka Peterson Maero aliwaonya vijana wanaokubali kuvuruga wakazi mjini humo na kusema kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria .
“Naomba kila kijana kufanya kazi ambayo itamsaidia maishani baada ya kutumiwa na wanasiasa kuleta mzozo hapa keroka,” alisema Maero.
“Vurugu za kila mara hazisaidii chochote, ila ni kuleta utata na kutokuwa na amani mwongoni mwa wanachi, natoa ushauri kwa kila kijana kujihusisha katika masuala ya usaidizi haswa biashara ili kujinufaisha,” aliongeza Maero.
Mzozo umekuwa ukishuhudiwa mpakani Keroka, jambo ambalo limeshukiwa kuwa la kisiasa huku magavana wa kauti hizo wakiombwa kutatua changamoto hizo kukomesha mizozo ambayo haina usaidizi.