Waziri wa Afya katika kaunti ya Nakuru Dkt Mungai Kabii amepongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuzindua rasmi mashine za kupima saratani. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza na wanahabari Alhamisi, waziri Kabii amesema kuwa mashine hizo ni hatua mwafaka. 

Ametoa wito kwa wakaazi kutumia fursa hii na kujitokeza kupimwa saratani. 

"Wakati ni sasa kwa wakaazi kujitokeza na kutumia mashine hizi kati vita dhidi ya saratani," akasema Kabii. 

Ni vyema kuashiria hapa kwamba mashine hizo zimezinduliwa na Rais Uhuru Kenyatta katika ziara yake ya kanda ya bonde la ufa.

Picha: Rais Uhuru Kenyatta katika hospitali kuu ya Bonde la Ufa Nakuru. Waziri wa afya Nakuru Mungai Kabii amewataka wakazi kutumia vyema mashine hizo. PMambili/Hivisasa.com