Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nyamira Alice Chae ameahidi kutenga pesa ili kupambana na dhuluma ya kijinsia kwa wanawake katika eneo hilo.

Kulingana na mbunge huyo, atatenga asilimia ishirini za pesa za hazina ya Affirmative Action Social Development ili kutumika kupambana na dhuluma hizo katika vijiji mbalimbali vya kaunti hiyo.

Akizungumza siku ya jumatano mjini Nyamira, Chae aliahidi kupigania wanawake na wasichana katika jamii mbalimbali ili kuhakikisha usawa wa kinjinsia.

“Kuna dhuluma ambazo huenezwa kwa wanawake na wasichana katika jamii zetu za Kisii. Mimi kama mwakilishi nimeungana nao ili kupigania haki kwa wanawake na wasichana,” alisema bi Chae.

“Nitatenga pesa asilimiaishirini za hazina ambayo tunaisimamia kama wawakilishi wa wanawake ili kutumika kupambana na dhuluma hizo kwa miji mbalimbali ,” aliongeza mbunge huyo.

Hata hivyo, aliwaomba wazee kuwaona wanawake kama sawia katika jamii na kuacha masuala ya kuwachapa kwani ni kinyume na sheria .

Chae pia aliomba wazazi wanaopeleka watoto wasichana ili wakeketwe kukomeza tabia hizo kabla ya kuchukuliwa hatua kali ya kisheria huku akitoa tahadhari kwao.

Mwakilishi huyo aliipongeza serikali ya kitaifa kwa kuunda hazina hiyo inayosimamiwa na wawakilishi wa wanawake wa kaunti ili kufanya maendeleo yao.