Wakazi wa Wadi ya Sensi eneo bunge la Kitutu chache wamemtaka mwakilishi wao Onchong’a Nyagaka kutembea katika wadi hiyo kuwaeleza miradi ya maendeleo amefanya tangu aingie mamlakani.
Kulingana na wakazi hao, ni haki yao kuelezwa miradi ya maendeleo ambayo imefanywa ili kuweka uzani uongozi wa viongozi wao.
Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano katika eneo la Sombogo, wakazi hao walimtaka mwakilishi wao kutembelea miradi ya maendeleo amefanya na kuwaeleza wakazi miradi hiyo moja kwa moja.
Ata hivyo, walimtaka mwakilishi wao kuwaeleza ni maendeleo gani ameratibu kufanya katika mwaka huu wa 2016.
“Tunaomba mwakilishi wetu akuje atembee kwa wadi hii atueleze yale ameyafanya tangu aingie mamlakani na yale amepanga kufanya mwaka ujao,” alisema Andrew Nyakoe, mkazi wa wadi ya Sensi.
Aidha, wakazi hao walimkosoa mwakilishi huyo kwa kutoweka miradi ya maji ambayo aliahidi hapo mbeleni, na kuchukua mda mrefu bila miradi hiyo kuanzishwa kufikia sasa.
“Nyagaka alituambia atapunguzia wanawake mzigo wa kutembea mbali kutafuta maji, akasema atachimba kisima eneo la Nyakeiri, Nyagoto, na maeneo mengine na hadi sasa hatujaona lolote likifanywa, ndio maana tunamhitaji hapa asimame atueleze.
Pia walimhitaji kukarabati baadhi ya barabara ambazo walisema ni mbovu, huku wakitumia mfano wa barabara ya Sombogo –Nyakenogo, Getare –Getenga miongoni mwa zingine.