Uhasama baina ya mwanamuziki Susumila na Tk2, ambaye ni mtayarishi wa ngoma, huenda ukachipuka upya baada ya Tk2 kususia kumtangaza Susumila kama mshindi wa tuzo za Vibe City zilizofanyika wikendi iliyopita.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mchakato huu ulianza pale ambapo Tk2 aliitwa kwenye jukwaa kumtangaza mshindi wa tuzo hilo, ila pindi tu ya kukabidhiwa bahasha la tuzo na kuliona jina la Susumila, mtayarishaji huyo wa ngoma zinazotamba hapa Kenya alikataa kusoma jina hilo.

Mtayarishaji huyo alimwambia Dj Chriss aliyekuwa akicheza ngoma ya Susumila kwa wakati huo kuendelea kucheza wimbo huo wa 'Ngoma Itambae' kwani aliyekuwa akiimba ndiye mshindi.

Tk2 ambaye ndiye aliyetayarisha ngoma hiyo, alikataa kumtaja Susumila hata baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mtangazaji mmoja wa Pilipili FM.

Uhasama huo ulianza kushuhudiwa mapema mwaka jana wakati wawili hao walipoitwa kwenye mahojiano na kituo cha Pilipili FM ambapo nusura warushiane makonde.

Hata hivyo, Tk2 alisema kuwa hana uhasama na Susumila katika maswala ya biashara, na kuongeza kuwa mambo mengine hataki kuweka hadharani.