Wahudumu wa pikipiki huko Mau Narok wametakiwa kuzingatia sheria za trafiki ili kuepuka ajali za kila mara eneo hilo.
Wito huo umetolewa na mwanaharakati wa kisiasa Ezekiel Kamau Ng'ang'a.
Akizungumza mapema Jumanne, eneo hilo wakati alipowapelekea wahudumu hao mavazi ya usalama maarufu 'reflector Jackets', Kamau alisema kuwa ajali nyingi zaweza kupunguzwa iwapo sheria za trafiki zitazingatiwa.
"Langu ni kuwarai tu kwamba tuweze kuzingatia sheria za trafiki ili kuepuka ajali nyingi za barabarani," alisema Kamau.
Wakati uo huo, aliwataka maafisa wa trafiki kutowahangaisha wahudumu wa pikipiki kila mara.
Zaidi ya wahudumu wa pikipiki 500 walipokezwa mavazi hayo ya reflector lengo ikiwa ni kuhakikisha usalama wao.