Wanaume watatu wamefikishwa katika mahakama ya Winam jijini Kisumu siku ya Alhamisi kujibu shtaka la kuiba ng’ombe.
Upande wa mashtaka umefahamisha mahakama kuwa mnamo tarehe Septemba 13, 2013, watatu hao, Kevin Otieno, Edwin Otieno na Wyckliffe Aura wakiwa eneo la Wathorego jijini Kisumu waliiba ng’ombe wenye thamani ya shilingi elfu 150 mali ya mlalamishi Seline Angeline.
Wakiwa mbele ya hakimu Edward Kori, washtakiwa wamekanusha mashtaka dhidi yao.
Kutokana na kutokuwepo mashahidi wa kutosha Korir alihairisha kesi hiyo na kuamua kusikilizwa tena mnamo tarehe Aprili, 25 2016.