Share news tips with us here at Hivisasa

Idara ya Afya katika Kaunti ya Mombasa imeanzisha ukaguzi kwa kampuni zote za kutengeneza maji ya chupa, ili kuhakikisha maji hayo ni salama kwa matumizi ya wananchi.

Kulingana na Mkuu wa Idara ya Afya katika Kaunti ya Mombasa Mohammed Abdi, ukaguzi huo utaendelezwa hata katika shule na vibanda vya chakula, ili kuhakikisha maji yanayotumiwa ni salama kama njia moja ya kuwakinga wakaazi dhidi ya ugonjwa wa homanyongo (A).

Hatua hiyo inajiri kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa homanyongo (A) katika baadhi ya sehemu za Kaunti ya Mombasa ambapo kufikia sasa zaidi ya watu 50 wameathirika kutokana na ugonjwa huo.

Aidha, Abdi alisema kuwa hali ya wakaazi kunywa maji yasiyosafi ndiyo inaonekana kusaidia uenezaji wa ugonjwa huo, na kusisitiza umuhimu wa hali hiyo kudhibitiwa vilivyo.