Mamlaka ya kudhibitisha bidhaa nchini KEBS imesema wananuia kufungua afisi zake katika kaunti ya Mombasa ili kuboresha utendakazi wake katika eneo hilo na haswa katika kunasa bidhaa gushi katika bandari ya Mombasa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Charles Ongwae amesema kuwa tayari mamlaka hiyo ishanunua ardhi ya kujenga afisi zake na zoezi nzima ya kutathmini bajeti ya kujenga ofisi hizo ishaanza.

“Tunatarajia kuwa zoezi nzima itakamilika kufikia mwisho wa mwaka huu ili tuanze kazi katika kaunti ya Mombasa mara moja," Ongwae alisema siku ya Ijumaa katika kongamano la washikadau wa sekta ya biashara za kibinafsi katika kaunti ya Mombasa.

Mamlaka hiyo pia inanuia kufungua afisi zake katika kaunti ya Kisumu na kaunti ya Uasin Gishu ili kuboresha utendakazi wake katika maeneo hayo.