Mahakama ya Mombasa Ijumaa iliwapata na hatia waethiopia wanne kwa kuwemo nchini bila stakabadhi zinazotakiwa na ikawapa kifungo cha mwaka mmoja gerezani au faini ya laki moja ili wasindikizwe kwao nchini.
Kwa mujibu wa Baraka FM, Gibra Gabero, Gazain Gargino, Zagei Demage na Adimo Hailemarain walifungwa kifungo hicho baada ya kukiri mashtaka yao mbele ya Hakimu mwandamizi Henry Nyakweba.
Mahakama hiyo iliambiwa ya kwamba wanne hao waliokamatwa Juni 29 kule Likoni wakiwa na wengine walipatikana wakiwa hawana pasipoti wala stakabadhi zozote za kuwepo nchini.
"Watuhumiwa walikuwa nchini kinyume cha sheria zilizowekwa na hakuna mmoja ametoa malilio ya kwa nini wasiadhibiwe kwa makosa yao," hakimu alisema.
Hakimu Nyakweba aliwapa muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.