Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Kaunti ya Mombasa kuhusu Fedha, Makadirio ya Bajeti na Uchumi Mohammed Khatimy amesema kuwa wakaazi wa kaunti hiyo hawana ufahamu wa katiba.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea na wanahabari afisini mwake mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Khatimy alitoa mfano wa kifungu kinacho orodhesha majukumu ya serikali za ugatuzi na yale ya serikali ya kitaifa, na kusema kuwa wakaazi wengi hawajajua majukumu ya serikali hizo mbili.

Khatimy alisema kuwa ana kumbana na changamoto kubwa wakati wa kuchukua maoni ya kushirikishwa katika bajeti ya mwaka wa 2016/2017, kwani maswala mengi yanayowasilishwa na wakaazi hao sio majukukumu ya serikali za kaunti.

“Kweli tunapitia changamoto nyingi sana wakati wa kukusanya maoni ya wakaazi ili kutusadia kutengeza bajeti yetu ya kaunti kutokana na kuwa wengi wa wakaazi hawafahamu katiba na majukumu ya serikali kuu na zile za kaunti. Tuko na jukumu kubwa sana la kuwaelimisha mwanzo ndio tukusanye maoni,” alieleza Khatimy.

Aidha, aliwataka wakaazi hao kujitokeza watakapokuwa wakiwahamasisha kuhusu katiba, ili kuhakikisha kuwa wanapata ufahamu wa katiba na kufahamu mengi kuhusu majukumu ya serikali za kaunti.