Mkurugenzi mkuu wa shirika la kutathmini ubora wa bidhaa nchini (KEBS) Charles Ongwae amewataka wafanyibiashara na washikadau kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingia na zinazouzwa nchini zimeafikia viwango vya ubora na kuidhinishwa na shirika hilo.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Ongwae alisema kuwa shirika hilo linapania kujenga maabara mjini Mombasa ili waweze kurahisisha kazi ya kutathmini bidhaa zinazoingia humu nchini, ikizingatiwa kuwa Bandari ya Mombasa ndio inayoingiza bidhaa nyingi nchini.
Aidha, Ongwea ameongeza kuwa shirika hilo litatoa alama na viwango vipya, ili waweze kutofautisha na zile alama za awali.
Wakati huo huo, mwenyekiti wa shirika hilo Lucas Maitha amewaonya wafanyibiashara wanaoingiza bidhaa ghushi kuwa watakabiliwa na sheria.
Maitha aidha alisema kuwa wafanyibiashara hao wana hadi Julai mosi kutuma maombi ya alama mpya katika makao makuu ya shirika hilo.