Mbunge wa bunge la Africa Mashariki Joseph Kiang'oi amejitokeza kutangaza wazi azma yake yakuwania useneta katika kaunti ya Nyamira.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubia wanahabari kule Riomego wakati wa hafla yakuchangisha pesa za paroka ya kanisa katoliki la Riomego, Kiang'oi alisema kuwa atawania useneta mwakani ili kubadilisha hali ya uongozi katika kaunti hiyo.

"Leo natangaza wazi kwamba nimejitoza rasmi kwenye kinyanganyiro chakuwania useneta katika kaunti hii kwa maana nina hamu yakubadilisha hali ya uwakilishi kwenye seneti," alisema Kiang'oi.

Kiang'oi ambaye aliwahi kuwa mbunge wa eneo bunge la Mugirango Kaskazini aidha alimshtumu seneta wa kaunti ya Nyamira Okong'o Mong'are kwa uongozi duni huku akimtaka kuwasilisha mahitaji ya kaunti bungeni.

"Useneta ni cheo cha muhimu sana katika kuamua ni kiwango kipi cha pesa zinazokuja katika kaunti kwa maana seneta ndiye anayestahili kuwasilisha mahitaji ya kaunti," alisema Kiang'oi.

"Ila seneta Mong'are amefeli kwa maana hadi sasa kaunti ya Nyamira haijakuwa ikipokea mgao wakutosha kutoka kwa serikali ya kitaifa," aliongezea Kiang'oi.