Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka Ishirini na mitano ameuawa huko Kisauni mapema leo kwa kupigwa risasi na afisaa wa polisi.
Mwanamume huyo anayeshukiwa kuwa mwanachama wa kundi linalotekeleza maovu kwa kuwapora na kuwauwa wenyeji la Wakali kwanza ameuawa katika eneo la Msikitini- Magodoroni alipokuwa akijaribu kumuibia mama aliyekuwa akisafiri kwenye gari.
Kulingana na walioshuhudia washukiwa wengine kumi waliokuwa wamejihami kwa silaha wamefanikiwa kukwepa mtego wa polisi huku mshukiwa mmoja akipata jeraha kwenye goti.
Aidha, mshirikishi wa kanda ya Pwani Nelson Marwa aliwaweka wazi wanaotekeleza uhalifu katika maeneo ya Kisauni haswa kundi la Wakali Kwanza na kuwataka polisi kuwachukulia hatua kali watakaopatikana .
Wiki jana Marwa aliwahakikishia wakazi wa Kisauni kuwa serikali itaimarisha usalama eneo hilo.
Kundi la Wakali Kwanza limekuwa likitekeleza uhalifu saa za mchana ambapo huwasimamisha wanaoendesha magari madogo aina ya tex na kuwaporwa kwa kuwatishia kwa bunduki