Mtu mmoja alifariki na wengine wawili kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali iliyotokea kwenye barabara kuu ya Nakuru kuelekea Nyahururu, Alhamisi asubuhi.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Bimam kwenye mteremko wa Maili Kumi hatua chache kutoka shule ya upili ya Jomo Kenyatta.
Ajali hiyo ilisababishwa na Ambulesi iliyokuwa ikielekea mjini Nakuru, baada ya gari hilo kugonga pikipiki iliyokuwa imebeba wateja wawili, kutoka kituo cha kibiashara cha Bahati.
Mteja mmoja alifariki papo hapo, huku mhudumu huyo wa bodaboda pamoja na mteja wake wa pili wakipata majeraha.
Maafisa wa polisi kutoka eneo la Bahati walifika katika mahala pa ajali na kuondoa mwili, na kuwapeleka waliojeruhiwa hospitalini.
“Ambulensi ilikuwa kwenye mwendo wa kasi, na barabara hiyo ina mashimo yanayokarabatiwa” akasema shahidi John Kamau
Gari hilo lilitumiwa kubeba walioumia, na hatimaye kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Bahati.