Maafisa wa polisi wilayani Borabu, kaunti ya Nyamira wamehimizwa kuzuia wizi wa ng’ombe ambao umekita mizizi wilayani humo.
Ombi hilo limetolwa baada ya visa hivyo kuongezeka, huku mkazi mmoja akipiwa na wezi wa ng’omba hadi kufariki siku ya Jumatano usiku alipotoka nje kukimbizana na wezi hao katika eneo la Isoge .
Wakizungumza siku ya Alhamisi katika eneo hilo la Isoge, wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na James Motari na George Morara waliomba maafisa wa polisi wa Borabu kuwasaidia kuzuia visa hivyo.
Aidha, waliomba kuimarishiwa usalama wao haswa nyakati za usiku kwani kufikia sasa ni wengi wamejeruhiwa na wengine kupoteza maisha yao kupitia wezi wa mifugio hao.
“Hapa Borabu tumekuwa na wizi ng’ombe na sisi maisha yetu tumehofia sana, tunaomba polisi kujaribu kila wawezalo kujali maslahi yetu na kutusaidia,” alisema Morara.