Wakaazi wa wadi ya Bahati katika kaunti ndogo ya Nakuru Kaskazini, wamempongeza mwakilishi wa wadi hiyo Peter Nderitu kufuatia maendeleo aliyofanya katika wadi hiyo haswa ya kukarabati barabara.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi waliozungumza na mwandishi huyu katika kituo cha Kibiashara cha Maili Kumi, walipongeza mwakilishi wao wa wadi, serikali ya kaunti pamoja na serikali ya Jubilee kwa kazi nzuri.

“Jubilee inafaa kongole angalau tunaona mabadiliko ya ugatuzi. Barabara hata kama si zote zimetengenezwa, zile ambazo zimekarabatiwa zinasaidia sana uchukuzi wa bidhaa,” John Kamau mhudumu wa boda boda alisema.

Naye Christine Wanjiku alisema:  “Kile nimefurahia sana ni ujenzi wa madarasa ya chekechea , kama lile lilijengwa katika shule ya Our lady, na linalojengwa huko Baraster.”

Kati ya miradi mingine ambayo imetekelezwa katika wadi hiyo, ni ujenzi wa hospitali, maji katika baadhi ya maeneo kama Landimawe, taa za usalama na usambazaji wa basari.

“Kazi tutafanya hata kama tunapigwa kisiasa na baadhi ya watu. Hatuwezi kamilisha yote katika mwaka mmoja wa kifedha, lakini tunazingatia kwanza miradi ambayo ina umuhimu kwa wakaazi,” MCA Nderitu alisema.