Wanafunzi zaidi ya hamsini waonaotoka kwa familia zisizo jiweza katika kaunti ndogo ya Nyakach wana kila sababu ya kutabasamu baada ya shirika moja lisilo ya serikali kuahidi kuwafadhili.
Shirika la Magunga Foot Steps lililoko wilayani Nyakach limetoa kima cha shilingi milioni moja mwaka huu kuchangia katika kushughulikia kimasomo wanafunzi kutokea katika familia zisizojiweza kifedha wakiwemo mayatima katika eneo hilo.
Afisa mshirikishi wa shirika hilo Rashid Mirika, amesema wamekuwa wakishughulikia masuala ya ujenzi ya shule na hospitali zilizoko Nyakach na kwa sasa wameanza mradi wa kusaidia watoto wanaotoka kwa familia zisizojiweza.
Mirika ameongeza kuwa kando na kulipia karo wanafunzi hawa wa shule za mshingi, upili na vyuo anuwai vile vile wanatia juhudi kuwanunulia na sara za shule miongoni mmwa mahitaji mingine.
''Vile vile kama shirika tumeweka mipango ya kuhakikisha wanafunzi walio katika shule za msingi wanapata lishe bora,'' alisema Rashid.