Askofu wa kanisa la Evangelica Lutherlan ELCK tawi la Nyamira mjini Thomas Obare amewahimiza wakristo kuwasaidia mayatima hasa kwa kuwalipia karo ya shule. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kwenye mahojiano kwa njia ya simu mapema Ijumaa, Obare alisema kuwa yafaa wakristo wajitokeze kuwasaidia watoto mayatima katika jamii hasa wale walio na upungufu wa kifedha. 

"Ndoto za watoto wengi hasa mayatima huzimwa kwa sababu hawewezi mudu kujilipia karo,  na ndio maana  nawahimiza wakristo kujitokeza kuwasaidia mayatima hasa kwa kuwalipia karo," alisema Obare. 

Obare aidha aliongeza kwa kuwarahi wazazi kutowaruhusu wanao kutazama vipindi kwenye runinga ambavyo vinaweza kupotosha maadili miongoni mwa vijana.

"Kwenye msimu huu wa pasaka, watu wengi hujivinjari kwa njia mbalimbali, ila ni ombi langu kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanawaelekeza wanao kwa njia zinazostahili hasa kwa kutowaruhusu kutazama vipindi ambavyo vinaweza kupotosha maadili," aliongezea Obare.