Wakaazi eneo la Mombasa wanaunga mkono shinikizo la muungano wa chama cha Cord kutaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuvunjiliwa mbali.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongozwa na mwanaharakati kutoka eneo hilo Musa Abdi amesema kuwa kwa kweli makamishna wa tume hiyo basi kuwa madai wanayoyatoa hao kuwa ni ya halali na hivyo basi ni sharti watoke afisini.

Licha ya kamishna wa IEBC Mohamed Alawi kukashifu hatua ya muungano wa Cord kwa kueneza madai ya uongo hadharani dhidi ya tume hiyo, Alawi amewataka viongozi wa Cord wakiongozwa na kinara wao Raila Odinga kuwashirikisha pale wanapohisi pana stahili kufanyiwa marekebisho kisheria badala ya kueneza uvumi usiokuwa na msingi.

Makamishna wa IEBC wakiongozwa na mwenyekiti wake Isaack Hassan hapo jana walisema kamwe hawatajiuzulu, na kumtaka kinara wa Cord Raila Odinga kuwasilisha ushahidi alionao kuhusu wizi wa kura wakati wa uchaguzi mkuu uliopita mwaka wa 2013.

Aidha wakaazi hao wamesema kuwa kauli zao walizozitoa hazitoshi kwao hao kama Wakenya wazalendo basi watoke na wapishe uchunguzi ufanyike.

Hata hivyo kilichowakera wakaazi hao kwa sana ni pale ambapo tume hiyo ilitupilia mbali zile sahihi ambazo chama hicho ilikuwa imekusanya iliziweze kuwezesha kufanyika kwa kura ya maaoni kuhusiana na kufanyia marekebisho katiba.

Itakumbukwa kuwa eneo la Pwani ni ngome ya chama cha Cord na hivi majuzi tu ambapo waliwapiku wenzao wa chama cha JAP kwenye uchaguzi mdogo wa Malindi na kumfanya Willy Mtengo kuwa mbunge wa eneo hilo.