Mwenyekiti wa elimu katika kaunti ya Kisii Henry Onderi amewaonya wenyekiti wa bodi za shule katika kaunti hiyo dhidi ya kutumia nguvu kupita kiasi kwa kutishia walimu wakuu katika shule mbalimbali.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Onyo hilo limetolewa baada ya wenyekiti hao kumaliza majuma mawili tangu kuchaguliwa katika nyadhifa hizo wanazowakilisha huku ikibainika kuwa baadhi yao wameanza kutishia walimu kuwafuta kazi ikiwa hawatafanya wanavyotaka.

Akizunguma siku ya alhamisi katika eneo la Nyantaro, Onderi alisema katiba iliyopitishwa mwaka wa 2010 itatumikwa kuwachukulia hatua kali wenyekiti wa bodi za shule ambao wana tabia za kutishia walimu wakuu bila kosa lolote.

“Tumepata habari kuwa baadhi ya wenyekiti wa bodi za shule wameanza kutishia kuwafuta walimu wakuu wa shule bila kosa lolote," alisema Onderi.

 "Naomba hiyo tabia ikomeshwe au wachukuliwe hatua kali za kisheria maana tuko na katiba ya kutetea walimu ambao hawana makosa,” alisema Onderi.