Jina Miss Diva kwenye vipindi vya radio hapa Pwani bila shaka huwarausha wengi wanaoenda kazini na hata wale wanaotegea tu kusikia sauti ya binti huyu akichambua maswala yanayoikumba jamii kila siku saa kumi na mbili hadi nne asubuhi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Jina lake halisi ni Nelly Mwikamba, mtangazaji mchapa kazi katika kituo cha radio cha Pilipili FM, mojawapo ya vituo vinavyojumuisha kampuni ya Mediamax.

Akiwa mwenye maswala mengi ya kuelimisha jamii, Miss Diva alianza kazi yake katika kituo cha Baraka FM anakoaminika kupata umahiri mkubwa, hasa baada ya kutwaa asilimia kubwa ya wakazi wa Pwani alipokuwa kwenye kipindi cha mchana.

Kazi yake kuu ilikuwa kuwaburudisha wasikilizaji kwa gumzo kidogo kama ilivyo wakati wa mchana.

Mwikamba alihamia Pilipili FM ambako alikutana na vijana wachapa kazi wenzake ambao walijumuisha kikosi ambacho kufikia sasa kinazidi kutwaa anga za Pwani kwa kipindi chao cha asubuhi, huku mwanadada huyo akiwa kipenzi cha wasikilizaji wengi.

Chris, al maarufu Man with the base na Chigulu Ngala wanajumuisha timu ya masongora watatu wanaowazindua wakazi wa Pwani kutoka usingizini kwa kipindi Zinduka na kahawa uthungu kila siku ya wiki.

Kipindi hicho kimemfanya Mwikamba kuwa tamanio la tena na tena kwa wasikilizaji kuendelea kutegea mita bendi za Pilipili bila ya sababu maalumu, kutokana tu na vile anavyotamka na anavyoweka mjadala wazi hewani na namna anavyochanganua kwa uwazi na ukweli bila kuegemea upande wowote.

Yote tisa Mwikamba ni mwanadada mwenye familia na hupenda sana kufurahia na familia yake hasa kila akitoka kazini.