Mshukiwa wa ujambazi aliyenaswa na bunduki inayoripotiwa kuibiwa kutoka kwa Kituo cha polisi cha Likoni, ameachiliwa kwa dhamana ya shillingi laki tano.
Rama Ali Bamama, anakabiliwa na mashtaka manne ya kupatikana na bunduki aina ya G3 na risasi moja bila kibali.
Bamama alitiwa mbaroni tarehe Oktoba 3, mwaka huu katika eneo la Majengomapya, Likoni.
Mshukiwa huyo hata hivyo alikanusha mashtaka yote mbele ya Hakimu mkuu Julius Nange'a.
Hakimu Nange'a alimuachilia kwa dhamana ya shilingi laki tano.
“Mshukiwa amekanusha mashtaka yote, basi mahakama inamuachilia kwa dhamana ya shilingi laki tano,” alisema Nange'a.
Kesi hiyo itatajwa Oktoba 27, mwaka huu.